Agosti 6, 2011, Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa alitoa taarifa yake kuhusu kile ambacho ameshakifanya ili kuleta maendeleo jimboni mwake mbele ya wajumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM ya wilaya ya Ruangwa.
Mbali na wajumbe hao wa CCM, walikuwepo pia viongozi wa idara mbalimbali za Halmashauri ya Ruangwa wakiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Hawa Mchopa.
Mbunge huyo alibainikisha ambacho amekifanya kwa zaidi ya miezi sita ikiwa ni pamoja na kusaidia kuinua kiwango cha elimu jimboni mwake kwa kuwalipia ada baadhi ya wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo.
Majaliwa pia aliezea misaada mbalimbali ikiwemo ya kibinadamu ambayo ameitoa kwa wahitaji achaguliwe kushika nafasi hiyo ambapo wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM waliipokea kwa kishindo.
Wajumbe hao waliichukulia taarifa hiyo kama mfano wa kuigwa huku wakidai kuwa Majaliwa amekuwa mbunge wa kwanza jimboni humo kufanya kazi na kisha kuitolea taarifa sahihi isiyo na maswali.
No comments:
Post a Comment