Thursday, September 1, 2011

Mheshimiwa Kassim Majaliwa (kulia) akipokea vitabu kutoka kwa Nyambari Nyangwine.


Mbunge wa Jimbo wa Ruangwa azidi kuimarisha elimu jimbo mwake.

Shule za msingi na sekondari za wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi,  kupitia kwa mbunge wa Jimbo la Ruangwa, mheshimiwa Kassim Majaliwa zimeendelea kufaidika kwa kupata msaada wa vitabu mbalimbali.
Kwa mara ya kwanza zilipata vitabu 900 kutoka Maktaba Kuu ya Taifa na sasa zimeendelea kupata msaada wa vitabu vingine 500 vilivyotolewa na kampuni za Nyambari Nyangwine za jijini Dar es Salaam.
Vitabu hivyo tayari vimeshakabidhiwa kwa mheshimiwa Majaliwa ambaye sasa anajiandaa kwenda kuvigawa kwenye jimboni mwake.
Mbali na vitabu hivyo kampuni za Nyangwine pia zimemkabidhi mbunge hiyo limu tatu ambazo zinatengezwa na kampuni hiyo.
Aidha, akitoa msaada huo, mkurugenzi wa kampuni hizo Nyambari Nyangwine aliahidi kuendelea kumsaidia mheshimiwa Majaliwa kwa vitabu mbalimbali ili kuhakikisha kwamba jimbo lake linainuka kielimu.

Wednesday, August 17, 2011

Hivi ndivyo wasafiri wa mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara wamekuwa wakikutana nayo hasa kipindi cha mvua kufuatia kipande cha barabara cha kilometa 60 kutoka Nyamwage hadi Somanga kutokuwa na lami ambapo magari yamekuwa yakikwama njiani kwa muda mrefu na kusababisha usumbufu.


Wilaya ya Ruangwa imeanza ujenzi wa maghala yatakayotumika kuhifadhi mazao mbalimbali ya wakulima. Pichani wakazi wa jimbo la Ruangwa wakiwa kwenye moja ya msingi wa maghala hayo ambapo mbunge wa jimbo hilo, Kassim Majaliwa ameshahimiza ujenzi wake kufanyika haraka.


Huku ndiko mheshimiwa Kassim Majaliwa alikoanzia hadi akawa mbunge wa jimbo la Ruangwa na kisha Naibu Waziri. Hapa akinadiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya makamu wa rais, Dk. Gharib Bilal kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akiwa na mgeni wake Mkurugenzi wa kampuni ya Planet Minerals International ya Marekani, Imat Eddi Wadi aliyeshika mfuko wa korosho zinazobanguliwa na kikundi cha Wabangua Korosho Ruangwa (WAKORU). Mbunge huyo amekuwa akifanya juhudi za kutafuta wawekezaji kufika jimboni humo ili kuona jinsi ya kuwekeza kwa ajili ya maendeleo ya Ruangwa.


Tuesday, August 16, 2011

Mbunge wa jimbo la Ruangwa ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Elimu, Kassim Majaliwa (kulia) akipokea baadhi ya vitabu vilivyotolewa na Maktaba Kuu ya Taifa kwa ajili ya shule za wilaya ya Ruangwa toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa maktaba hiyo Alli Mcharazo.


Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa aendelea kusaidia sekta ya elimu jimboni mwake

Baadhi ya wakazi wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi wamediriki kusema kuwa sasa wamepata mbunge ambaye kwa muda mrefu walikuwa wakimhitaji awawakilishe bungeni.
Hii inatokana na makubwa ambayo mbunge wao, Kassim Majaliwa amekuwa akiyafanya kwa kipindi kifupi ambacho amechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Hili limeendelea kuonekana kwa jinsi ambavyo amekuwa akihangaika huku na huko ili kuhakikisha kwamba jimbo hilo linapata maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu.
Hivi karibu mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia elimu alipokea vitabu 900 kwa ajili ya shule 20 za wilaya ya Ruangwa.
Vitabu hivyo vilitolewa na Maktaba Kuu ya Taifa na Mkurugenzi wake, Alli Mcharazo na kukabidhiwa kwa mheshimiwa Majaliwa ili akavigawe kwa shule 20 zikiwemo 10 za msingi na 10 za sekondari.
Mheshimiwa Majaliwa anatarajia kupeleka vitabu hivyo mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu wa 2011 ambapo pia mbunge huyo ana mpango wa kutoa jengo litakalotumika kama maktaba ya wilaya.
Kwa hatua hii na mengine mengi ambayo amekuwa akiyafanya kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa jimbo lake, baadhi ya wananchi wamesema kuwa huyo ndiye mbunge waliyekuwa wakimhitaji kuwa mwakilishi wao bungeni.


Tuesday, August 9, 2011

Wanafunzi nao wamekuwa wakifaidika na misaada ya mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa. Hapa akiwapa mpira wanafunzi wa Shule ya Msingi Chinongwe.


Baadhi ya wakazi wa jimbo la Ruangwa wamekuwa wakijishughulisha na ufugaji kama ambavyo picha hii inaonyesha kijana wa kata ya Chinongwe jimboni humo akichunga ng'ombe na mbuzi.


Baadhi ya askari wa polisi wa kituo cha Ruangwa wakiwa kwenye kikao maalum kilichoitishwa na mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa ili kuzungumzia masuala ya ulinzi na usalama.


Hapa picha za matukio tofauti ambayo mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa amekuwa akiyafanya awapo jimboni humo huku akishuhudiwa na wananchi wake.


Hii ni barabara kuu inayoingia mjini Ruangwa mkoani Lindi mji ambao unaendelea kukua kutokana na mwingiliano wa watu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wanaoingia kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za uchimbaji dhahabu eneo la Namungo kata ya Mbekenyera.


Jimbo la Ruangwa kama yalivyo majimbo mengine limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za ubovu wa miundombinu ya barabara. Hapa mwendesha pikipiki akijaribu kuvuka kwenye maji yaliyochanganyika na tope.


Monday, August 8, 2011

Mbunge wa jimbo la Ruangwa amekuwa mstari wa mbele kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi wake pale wanapokuwa na matatizo. Hapa akikabidhi moja ya msaada wa unga kwa diwani wa kata ya Chinongwe, Fabian Nguli kwa ajili ya wakazi wa kata yake.


Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa (kulia) akimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hawa Mchopa alipokuwa akielezea hali halisi ya maendeleo ya wilaya hiyo wakati mbunge huyo na ujumbe wake walipomtumbelea ofisini kwake.


Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa akikabidhi msaada wa mashati kwa mmoja wa mzee wa kijiji cha Liuguru, Rashid Liwanje ili agawane na wenzake, alipotembelea kata ya Chunyu kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao bungeni.


Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa anapwapo jimboni humo hutembelea vijiji mbalimbali ili kuwajulia hali wananchi wake. Pichani akifurahia jambo na mkazi wa kijiji cha Nandandala.


Baadhi ya wakuu wa Idara mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wakijadiliana nje ya ukumbi wa jengo la chama cha walimu wilayani humo baada ya taarifa yao ya shughuli za maendeleo kukataliwa na wajumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo.


Hekima ya mbunge Kassim Majaliwa yawaokoa wakuu wa Idara za Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa

Wakuu wa idara mbalimbali za Halmshauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, walijikuta katika wakati mgumu kufuatia taarifa yao ya shughuli za maendeleo kukataliwa na wajumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo.
Tukio hilo lilitokea Agosti 6, 2011 katika ukumbi wa jengo la Chama cha Walimu wilayani humo mara baada ya Afisa Mipango wa wilaa hiyo Godfrey Lwambano kusoma taarifa hiyo ndipo ukafika wakati wa kuijadili.
Kwenye majadiliano hayo ilibainika kuwa kilichosomwa na Afisa huyo haikuwa na ukweli wowote na hasa kuhusu miradi ya maendeleo, mikopo kwa vikundi mbalimbali wakiwemo wanawake na vijana na mambo mengine.
Hali hiyo ilisababisha kuzua maswali mengi magumu ambayo wakuu wa idara walikuwa na majibu mepesi na kusababisha malumbano makali hadi mbunge wa jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa alipoingia kati kuokoa jahazi.
Bila hekima ya mbunge huyo, wakuu hao wa idara walikuwa na wakati mgumu kujibu makombora yaliyoelekezwa kwao na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ambao walukuwa na kiu ya kutaka kupata ukweli kuhusu taarifa hiyo.
Baada ya kuona mambo yanakwenda ndivyo sivyo, mbunge huyo aliingilia kati na kuwaambia wakuu hao wa idara kuwa taarifa yao ilijaa maswali mengi kuliko majibu na kushauri kuwa ikaandaliwe upya.
Ushauri huo wa mbunge ulipokelewa kwa shangwe na wajumbe hao ambapo wakuu wa idara walilazimika kuondoka kwenye kikao hicho ambapo sasa taarifa  yao huenda ikajadiliwa mwezi Septemba.

Hapa mbunge wa jimbo la Ruangwa ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Elimu, Kassim Majaliwa akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Stashahada ya Ualimu kwenye mahafali ya pili ya Chuo cha Chuo cha Ualimu Dakawa, mkoani Morogoro.

Sunday, August 7, 2011

Wajumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM wa wilaya ya Ruangwa wakifuatilia kwa umakiniwakati mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa alipokuwa akisoma taarifa ya kazi ambazo ameshazifanya kwa ajili ya maendeleo ya jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya kazi za maendeleo alizozifanya jimboni humo kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu amechaguliwa kuwa mbunge.

Mbunge Kassim Majaliwa atoa taarifa ya kazi zake kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo la Ruangwa

Agosti 6, 2011, Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa alitoa taarifa yake kuhusu kile ambacho ameshakifanya  ili kuleta maendeleo jimboni mwake mbele ya wajumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM ya wilaya ya Ruangwa.
Mbali na wajumbe hao wa CCM, walikuwepo pia viongozi wa idara mbalimbali za Halmashauri ya Ruangwa wakiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Hawa Mchopa.
Mbunge huyo alibainikisha ambacho amekifanya kwa zaidi ya miezi sita ikiwa ni pamoja na kusaidia kuinua kiwango cha elimu jimboni mwake kwa kuwalipia ada baadhi ya wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo.
Majaliwa pia aliezea misaada mbalimbali ikiwemo ya kibinadamu ambayo ameitoa kwa wahitaji achaguliwe kushika nafasi hiyo ambapo wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM waliipokea kwa kishindo.
Wajumbe hao waliichukulia taarifa hiyo kama mfano wa kuigwa huku wakidai kuwa Majaliwa amekuwa mbunge wa kwanza jimboni humo kufanya kazi na kisha kuitolea taarifa sahihi isiyo na maswali.

Thursday, August 4, 2011

Kwa umahiri wake na jinsi anavyopendwa na wakazi wa jimbo lake, mbunge Kassim Majaliwa anapofanya mikutano baadhi wanachama wa vyama vya upinzani wamekuwa wakirudi CCM. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, mzee Muya akipokea kadi ya CUF toka kwa mmoja wana CUF aliyeamua kujiunga CCM baada kufurahishwa na hotuba ya mbunge huyo.

Hata kwenye ngoma za asili, mheshimu mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa amekuwa akishiriki kuzicheza kama anavyonekana akicheza na baadhi ya wananchi wa kata ya Chunyu alipokwenda kuwatambelea.

Watu wanapokuheshimu ni muhimu wakufanyie jambo. Pichani mheshimiwa Kassim Majaliwa mbunge wa Jimbo la Ruangwa akikabidhiwa mkuki na wazee wa kimwera baada ya kuvishwa kofia, lubega na kupewa kigoda kama ishara ya kuwa mzee wa kimila wa kabila la wamwera.

Mbunge wa Jimbo la Ruangwa ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Elimu akila kiapo cha kutumikia taifa kwa nafasi hiyo mbele ya rais Jakaya Kikwete.

Wakazi hawa wa kata ya Namichiga, Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, wakifurahia hotuba ya mbunge wao Kassim Majaliwa kwenye moja ya ziara zake jimboni humo.

Wednesday, August 3, 2011

Mbunge Kassim Majaliwa amekuwa mstari wa mbele kuhimiza michezo jimboni mwake. Hapa akitoa vyetu kwa wahitimu wa mafunzo ya michezo mbalimbali yaliyofanyika jimboni humo hivi karibuni.

Hapa mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa (kulia ) akizungumza na baadhi ya viongozi wa kukindi cha wabangua korosho jimboni humo.

Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya na askari polisi mara baada ya kuzungumza nao.

Awapo jimboni mwake, mbunge Kassim Majaliwa hukutana na watu mbalimbali ili kusikiliza kero na matatizo yao kama anavyozungumza na huyu mlemavu wa macho.

Miongoni mwa maendeleo ya Jimbo la Ruangwa ni uanzishwaji wa kituo cha redio. Pichani mmoja wa watangazaji wa Radio Ruangwa akiwa kazini.

Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa (kushoto), akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Mzee Muya katika moja ya mazungumzo yao.

Ruangwa ni moja ya majimbo yenye ardhi nzuri ambayo inakubali mazao mbalimbali yakiwemo mahindi kama shamba hili lililopo kata ya Chienjele linavyoonekana.

Mbunge Kassim Majaliwa ni mtu anayependwa na watu wa kila rika jimboni mwake. Hapa akisalimiana na watoto alipokuwa katika kijiji cha Nanganga akielekea jimboni mwake Ruangwa mkoani Lindi.

Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa (kushoto) akiangalia jinsi wachimbaji wadogo wa Namungo kata ya Mbekenyera jimboni humo wanavyoisafisha dhahabu alipotembelea jimboni mwake.

Hapa mbunge Kassim Majaliwa wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi akisalimiana na baadhi ya wakazi wa jimbo hilo katika moja ya ziara zake jimboni humo.

Manaibu Mawaziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) na Agrey Manri wakiteta jambo.