Sunday, September 18, 2011
Thursday, September 1, 2011
Mbunge wa Jimbo wa Ruangwa azidi kuimarisha elimu jimbo mwake.
Shule za msingi na sekondari za wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, kupitia kwa mbunge wa Jimbo la Ruangwa, mheshimiwa Kassim Majaliwa zimeendelea kufaidika kwa kupata msaada wa vitabu mbalimbali.
Kwa mara ya kwanza zilipata vitabu 900 kutoka Maktaba Kuu ya Taifa na sasa zimeendelea kupata msaada wa vitabu vingine 500 vilivyotolewa na kampuni za Nyambari Nyangwine za jijini Dar es Salaam.
Vitabu hivyo tayari vimeshakabidhiwa kwa mheshimiwa Majaliwa ambaye sasa anajiandaa kwenda kuvigawa kwenye jimboni mwake.
Mbali na vitabu hivyo kampuni za Nyangwine pia zimemkabidhi mbunge hiyo limu tatu ambazo zinatengezwa na kampuni hiyo.
Aidha, akitoa msaada huo, mkurugenzi wa kampuni hizo Nyambari Nyangwine aliahidi kuendelea kumsaidia mheshimiwa Majaliwa kwa vitabu mbalimbali ili kuhakikisha kwamba jimbo lake linainuka kielimu.

Subscribe to:
Posts (Atom)