Jimboni Ruangwa
Tuesday, October 4, 2011
Mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa, kwa sasa amejikita zaidi kuinua kiwango cha elimu na kuboresha afya za wananchi wake ambapo hivi karibuni alipeleka vitabu, vifaa vya maabara kwa ajili ya shule na magodoro kwenye hospitali ya wilaya na vituo vya afya.
Hivi karibuni mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa alizindua tamasha la Michezo kwa Wote lililoshirikisha wanafunzi toka shule mbalimbali za msingi jimboni humo kama ambavyo picha hizi zinavyoonyesha.
Mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa akitoa msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vya hospitali, michezo na shule za sekondari jimboni mwake.
Mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa akiwa katika picha za matukio mbalimbali jimboni humo ambayo yanalenga kuliletea maendeleo.
Sunday, September 18, 2011
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi, Fatuma Mikidadi (kushoto) akikabidhi baiskeli kwa mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ruangwa, Adela Ng'onye huku makatibu wa UWT toka kata za wilaya hiyo wakishuhudia. Mbunge ghuyo amegawa baiskeli 250 kwenye wilaya zote za mkoa huo.
Mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mandawa na kuwataka wasome kwa bidii ili wafanikiwe kusonga mbele kimasomo.
Mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akiteta na mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Kaspary Mmuya alipotembelea Shule ya Sekondari Mbekenyera ambayo ina uhaba wa walimu hali inayosababisha wanafunzi wanakosa baadhi ya masomo.
Older Posts
Home
Subscribe to:
Posts (Atom)